Kitendo hiki si kwamba kinaenda kinyume na Sunnah tu, bali pia kinyume na maamrisho yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah ni kumzika maiti ardhini, si kumzika juu ya uso wa ardhi kisha kujenga juu ya kaburi lake. Sasa tukikadiria kwamba maiti amezikwa, je, hilo ni jengo la mstatili, ni shimo au ni kuba? Unakusudia nini unaposema kuwa ni pango?
Muulizaji: Pango lililochimbwa chini ya ardhi.
al-Albaaniy: Hilo ni sawa. Ikiwa ni chini ya ardhi, hilo ni paa la asili na ardhi yenyewe ni paa. Muhimu ni kwamba achimbiwe shimo ardhini na azikwe humo. Ikiwa kuna shimo la asili, basi maiti aingizwe humo na kufunikwa kwa mchanga na hivyo kusudio litakuwa limepatikana. Lakini ikiwa ni juu ya uso wa ardhi, haijuzu.
Muulizaji: Hapana… pango hili lina mlango na wanazika humo makumi ya watu.
al-Albaaniy: Haijuzu. Wewe punde kidogo umesema wanazika ndani ya ardhi?
Muulizaji: Ndiyo, liko ndani ya ardhi.
al-Albaaniy: Ni ndani ya ardhi kwa namna ya kwamba limefunikwa na mchanga juu yake?
Muulizaji: Hapana.
al-Albaaniy: Hapana, kama ni hivyo. Usichukue tu nusu ya maneno.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
- Imechapishwa: 10/12/2024
Kitendo hiki si kwamba kinaenda kinyume na Sunnah tu, bali pia kinyume na maamrisho yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah ni kumzika maiti ardhini, si kumzika juu ya uso wa ardhi kisha kujenga juu ya kaburi lake. Sasa tukikadiria kwamba maiti amezikwa, je, hilo ni jengo la mstatili, ni shimo au ni kuba? Unakusudia nini unaposema kuwa ni pango?
Muulizaji: Pango lililochimbwa chini ya ardhi.
al-Albaaniy: Hilo ni sawa. Ikiwa ni chini ya ardhi, hilo ni paa la asili na ardhi yenyewe ni paa. Muhimu ni kwamba achimbiwe shimo ardhini na azikwe humo. Ikiwa kuna shimo la asili, basi maiti aingizwe humo na kufunikwa kwa mchanga na hivyo kusudio litakuwa limepatikana. Lakini ikiwa ni juu ya uso wa ardhi, haijuzu.
Muulizaji: Hapana… pango hili lina mlango na wanazika humo makumi ya watu.
al-Albaaniy: Haijuzu. Wewe punde kidogo umesema wanazika ndani ya ardhi?
Muulizaji: Ndiyo, liko ndani ya ardhi.
al-Albaaniy: Ni ndani ya ardhi kwa namna ya kwamba limefunikwa na mchanga juu yake?
Muulizaji: Hapana.
al-Albaaniy: Hapana, kama ni hivyo. Usichukue tu nusu ya maneno.
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
Imechapishwa: 10/12/2024
https://firqatunnajia.com/makaburi-ya-chini-ya-ardhi-na-makaburi-juu-ya-ardhi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)