Maji yanayomrukia mtu chooni

Swali: Ni ipi hukumu ya maji yanayomrukia mtu anapokuwa anaosha dhakari yake au tupu yake ya nyuma chooni?

Jibu: Kimsingi ni usafi katika maji. Mtu akiwa na yakini kwamba maji yaliyomrukia yamenajisika kwa mkojo au kitu kingine, basi analazimika kuosha nguo na mwili wake kutokana na yale maandiko yanayoamrisha kujisafisha kutokamana na najisi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (04/203)
  • Imechapishwa: 09/06/2022