Maji madogo yasiyotosheleza wudhuu´ ambayo mtu anayahitaji

Swali: Nilikuwa msafiri na nikatayamamu na kuswali ´Ishaa ilihali nilikuwa na maji ya kunywa kwa sababu masafa yaliyobaki [katika safari yangu] bado ni marefu. Je, kufanya kwangu Tayammum na kuacha kutumia maji ni sahihi?

Jibu: Ndio, ikiwa unachelea kuwa maji yatakuwa madogo kwa haja yako endapo utatawadha nayo, wewe ni mwenye kupewa udhuru. Fanya Tayammum nayo. Una hukumu moja kama ya mwenye kukosa maji. Ama ikiwa maji ni mengi na wala huchelei kuwa yataisha, katika hali hii haijuzu kwako ku-Tayammum.

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا

“… kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum.” (05:06)

Wewe uko na maji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-8.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020