Jawabu sahihi ni kwamba haisemwi kuwa maiti wanasikia chochote isipokuwa kwa dalili. Msingi ni kwamba maiti hasikii chochote. Hii ndiyo asili, kama Allaah alivyosema:
إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ
“Hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu.” (27:80)
وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ
“… na wewe huwezi kuwasikilizisha waliyomo makaburini.” (35:22)
Kwa hiyo maiti hasikii chochote isipokuwa kile kilichotajwa kwenye Maandiko. Kama kilivyokuja kwa Maandiko ya kwamba maiti anasikia nyayo za viatu vyao wanapogeuka na kuondoka, basi hiki kimekuja kwa Maandiko maalum. Anasikia maswali, swali la Malaika wanapomuuliza kuhusu Mola wako ni nani na dini yako ni ipi, haya ni kwa Maandiko maalum. Vilevile kuhusu watu wa Badr imethibiti ya kwamba walisikia maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakiwa kwenye kisima. Hili pia limetawa kwa Maandiko. Kwa hiyo yaliyotamkwa kwenye Maandiko tunayathibitisha. Yale ambayo hayakuja kwa Maandiko hatuyathibitishi, kwa sababu msingi ni kwamba maiti hasikii chochote wala hajui kuhusu hali za dunia chochote. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atasemewa siku ya Qiyaamah pale baadhi ya watu watakapokuja kwenye hodhi na kufukuzwa. Atasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Maswahabah zangu, ummah wangu.” Ataambiwa: ”Hakika hujui waliyozua baada yako.”
Hivi ndivyo ilivyokuja katika Swahiyh. Hili linafahamisha kutokusihi kwa Hadiyth inayosema kuwa matendo yao yanaonyeshwa kwake. Ikiwa yeye hajui kuhusu hali za watu, basi mwingine ana haki zaidi ya kutojua. Kwa hakika maiti hisia yake imekatika na matendo yake yamekatika. Kwa hiyo hajui kuhusu watu. Lakini katika ndoto roho zinaweza kukutana pale waislamu wanapoziota. Huenda roho zikakutana ambapo maiti akazungumza na roho ya aliye hai katika mambo fulani. Hili huenda likatokea wakati fulani katika yale yanayohusiana na ndoto – Allaah ndiye anayejua zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1027/درجة-حديث-تعرض-علي-اعمالكم
- Imechapishwa: 09/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1027/درجة-حديث-تعرض-علي-اعمالكم
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/maiti-anasikia-au-hasikii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket