Mahari yanatimia mpaka mume amnunulie mke sanami/fanicha yote ya nyumba

Swali: Katika baadhi ya miji ndoa inatimia baada ya mume kuandika kila kitachokuwa ndani ya nyumba hiyo ya ndoa katika samani na vyenginevyo ili awe ni miliki ya mke wakati atapomtaliki. Wakati mwingine huenda mume akaambiwa kuandika pia vitu visivyokuwepo hivi sasa. Je, haya yanazingatiwa ni katika Shari´ah kwa sababu ndio desturi katika miji hiyo?

Jibu: Haya yanategemea na ada na desturi. Ikiwa kwa mujibu wao mahari hayatimii isipokuwa mume anaorodhesha vitu vyote vinavyotakiwa kuwa nyumbani ili baadaye iwe ni milki ya mke, inategemea na ada. Ama kumlazimisha kufanya hivo pasi na kuwepo desturi iliyozoeleka, ni jambo halifai.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1255
  • Imechapishwa: 30/09/2019