Madoa ya damu juu ya nguo ya kuswalia

Swali: Ambaye juu ya nguo yake kuna madoa ya damu aswali nayo au asubiri mpaka atapoletewa nguo safi?

Jibu: Aswali kutegemea na hali yake. Asiache swalah mpaka ukatoke nje wakati wake. Bali aswali kutegemea na hali yake asipoweza kuiosha au kuibadilisha kwa mavazi mengine yaliyo masafi kabla ya kutoka nje wakati [wa swalah]. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Ni lazima kwa muislamu kuosha kile kilichopatwa na damu au abadilishe nguo yake yenye najisi kwa nguo nyingine safi akiweza kufanya hivo. Asipoweza kufanya hivo basi aswali kutegemea na hali yake na wala hatoirudia. Hayo ni kutokana na Aayah tukufu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yale niliyokukatazeni basi jiepusheni nayo na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/398)
  • Imechapishwa: 26/09/2021