Swali: Ni ipi hukumu ya imamu anayewaswalisha watu pasina kufunika kichwa chake?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo. Kichwa sio katika vile viungo visivyotakiwa kuonekana. Wajibu ni yeye kuswali na shuka ya chini na shuka ya juu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiswali mmoja wenu ndani ya nguo moja hakuna juu ya mabega yake kitu.”

Lakini bora zaidi ni pale atapochukua mapambo yake na akakamilisha mavazi yake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila swalah.”[1]

Lakini akiwa katika nchi ambayo sio katika desturi zao kufunika kichwa basi hapana vibaya kwake kukiacha wazi.

[1] 07:31

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/405)
  • Imechapishwa: 26/09/2021