Madhehebu yetu ni madhehebu ya Salaf. Tunathibitisha sifa pasi na kushabihisha na tunamtakasa Allaah pasi na kukanusha. Haya ndo madhehebu ya maimamu wa Uislamu kama mfano wa Maalik, ash-Shaafi´iy, ath-Thawriy, al-Awzaa´iy, Ibn-ul-Mubaarak, Imaam Ahmad na Ishaaq bin Raahuuyah. Madhehebu haya ndio yaliyofutwa na Mashaykh kama mfano wa Fudhwayl bin ´Iyaadhw, Abu Sulaymaan ad-Daaraaniy, Sahl bin ´Abdillaah at-Twustariy na wengineo. Hakuna yeyote katika maimamu hawa ambaye anaonelea kinyume katika misingi ya dini. Kadhalika Abu Haniyfah. ´Aqiydah iliyothibiti kwake ni yenye kuafikiana na ´Aqiydah ya watu hawa, nayo ni yale yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Imaam Ahmad amesema:
“Allaah hasifiwi isipokuwa kwa yale aliyojisifia Mwenyewe au yale aliyomsifia kwayo Mtume Wake. Hatuvuki Qur-aan na Hadiyth.”
Haya pia ndio madhehebu ya wengineo. Hivyo tunawafuata Salaf katika jambo hili. Kwani wao ndio maimamu wajuzi zaidi inapokuja katika suala la kukanusha na kuthibitisha. Wao wanamuadhimisha Allaah na kumtakasa Allaah zaidi kutokamana na yale mambo yasiyostahiki Kwake. Hakika maana ya wazi yenye kufahamika katika Qur-aan na Sunnah hairudishwi nyuma kwa utata. Kuirudisha ni njia moja ya kukengeusha maandiko kutoka mahala pake stahiki. Wala haitakiwi kusema kwamba ni maandiko yasiyofahamika maana yake na wala hayafahamiki makusudio yake. Hili lingekumbushia wale wanaosoma Kitabu pasi na kukifahamu. Uhakika wa mambo ni kwamba ni Aayah zilizo waziwazi. Zinafahamisha maana tukufu na ya wazi iliyosimama kwenye nyoyo za wanachuoni.
- Muhusika: Imaam Swiddiyq Hasan Khaan al-Qanuujiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qatf-uth-Thamar, uk. 57-58
- Imechapishwa: 29/01/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
29. Matahadharisho ya Salaf juu ya falsafa
Falsafa ni ile iliozushwa na wanafalsafa katika mambo ya I´tiqaad kama kuthibitisha ´Aqiydah kwa njia yao wenyewe waliyozusha na kupuuza yale yaliyokuja katika Qur-aan na Sunnah. Salaf wametahadharisha falsafa na watu wake kwa njia mbalimbali kutokana na vile inapelekea katika shubuha na mashaka. Imaam Ahmad amefikia mpaka kusema: "Mwanafalsafa hafanikiwa…
In "Fath Rabb-il-Bariyyah"

Shaykh Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kaja na madhehebu mapya?
https://www.youtube.com/watch?v=vns1tm7ddk4 Amefariki (Rahimahu Allaah) hali ya kuwa ni fakiri hana mali yoyote, lakini ana ujira na thawabu, na kaeneza elimu, Da´wah na imedhihiri dini ya Allaah (´Azza wa Jalla). Kama amevyosema Allaah (Jalla wa ´Alaa):' هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ "Yeye…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"
01. Utangulizi wa ”Bayaan-ul-Ma´aaniy”
Huu ni utangulizi wa Imaam na Haafidhw ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy ambao aliandika juu ya kitabu chake katika madhehebu ya Maalik. Hapo kitambo Salaf (Rahimahumu Allaah) walikuwa na mazowea pindi wanapotunga tungo za Fiqh basi huanza na ´Aqiydah. Walikuwa wakiigawanya Fiqh mafungu mawili; Fiqh kubwa katika ´Aqiydah…
In "Bayaan-ul-Ma´aaniy"