Madhehebu ya watu kuhusiana na Allaah kuwa juu. Watu wana madhehebu mane katika hilo:

Madhehebu ya kwanza: Madhehebu ya Salaf wa Ummah na maimamu wao miongoni mwa Maswahabah, Taabi´uun, maimamu na wanachuoni. Madhehebu yao ni kwamba Allaah Yuko juu ya mbingu, amelingana juu ya ´Arshi na ametengana na viumbe Vyake.

Madhehebu ya pili: Madhehebu ya Mu´attwilah Jahmiyyah na vijukuu vyao. Madhehebu yao wanasema kuwa Allaah hayuko ndani ya ulimwengu na wala nje yake, hakutengana nao na wala hakuambatana nao, hayuko juu na wala hayuko chini. Wanamkanushia sifa mbili zenye kukabiliana ambazo chenye kuwepo ni lazima kipatikane katika moja kati ya sifa hizo mbili. Haya yanasemwa na wengi katika Mu´tazilah na wenye kuafikiana nao ikiwa ni pamoja na Ashaa´irah waliokuja nyuma. Maelezo kama haya hayaoneshi jengine isipokuwa kitu kisichokuwepo.

Madhehebu ya tatu: Madhehebu ya Huluuliyyah Jahmiyyah ambao wanasema Allaah kwa dhati Yake yuko kila pahali. Haya yamesemwa pia na an-Najaariyyah.

Kujengea juu ya hili Jahmiyyah wanakuwa na madhehebu mawili:

1- Madhehebu ya wakanushaji. Hawa ni wale wenye kupinga sifa zote mbili.

2- Madhehebu ya Huluuliyyah. Hawa ni wale wenye kusema kuwa Allaah amekita kwenye kila kitu – Ametakasika Allaah na wanayoyasema.

Madhehebu ya nne: Madhehebu ya mapote miongoni mwa wanafalsafa na Suufiyyah. Hawa wanasema kuwa Allaah yuko juu ´Arshi na Yuko kila mahala. Wanasema kuwa Allaah kwa dhati Yake yuko juu ya ´Arshi na kwa dhati Yake yuko kila mahala.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/402-403)
  • Imechapishwa: 19/05/2020