Madhara yanayopatikana kwa mwanamke kutumia dawa za kuzuia hedhi

Kwa ajili hiyo tunawaambia wanawake wasijitaabishe nafsi na dhamira zao. Hili – yaani kupata hedhi – ni kitu wameandikiwa wanawake. Hivyo akipata hedhi asifunge.

Yanayofanywa na baadhi ya wanawake kujaribu kuzuia hedhi katika mwezi wa Ramadhaan, ni kosa wanalolifanya. Kwa sababu imethibiti kwetu ya kwamba dawa hizi zinazozuia hedhi zina madhara na zinamwathiri mwanamke katika kifuko cha uzazi, damu, mifupa na mtoto. Leo tunaona watoto wenye hitilafu wamekuwa wengi. Baadhi ya madaktari wanasema kuwa sababu moja wapo ni haya madawa. Ni jambo linalojulikana mtoto kuzaliwa hali ya kuwa ana hitilafu ni tatizo kwa mtoto mwenyewe na wazazi wawili. Ni jambo lina madhara makubwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 05/08/2020