Madhara yake ni makubwa kuliko manufaa yake

Swali: Dada yangu anataka kujifunza kuendesha gari katika nchi hii [Uingereza] kwa sababu wakati mwingine kuna dharurah na hivyo anahitaji gari. Anataka kujifunza lakini sio kwa ajili ya kuendesha isipokuwa tu wakati wa dharurah. Je, inafaa kwake jambo hilo?

Jibu: Allaah amempa udhuru wa kutohudhuria swalah ya ijumaa na amempa udhuru wa kutohudhuria swalah ya mkusanyiko. Amedondosha kutoka kwake ulazima wa swalah ya ijumaa na swalah za mkusanyiko. Haya ni mambo ya wajibu yaliyodondoshwa. Nyinyi mnataka kumtoa nje kwa ajili ya jambo ambalo hapana shaka yoyote kuwa madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Usrah https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/ftawa-osrh-godian.mp3
  • Imechapishwa: 14/09/2022