Machukizo ya kunywa kutoka kwenye mdomo wa kiriba na chupa

Msingi ni makatazo na uharamu. Baadhi ya nyakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikunywa kutoka kwenye mdomo wa kiriba, jambo ambalo linafahamisha kuwa makatazo ni kwa njia ya machukizo na sio uharamu kwa maana ya kwamba mtu anapata dhambi. Kwa sababu ni katika mambo ya adabu na mtu kujiepusha na mambo yanayomdhuru. Kwa hivyo inakuwa ni jambo lenye kuchukiza na maelekezo katika kheri na manufaa. Haja ikipelekea kunywa kutoka kwenye mdomo wa kiriba basi machukizo yanaondoka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24034/حكم-الشرب-من-فم-السقاء
  • Imechapishwa: 23/08/2024