Machukizo ya kukataa zawadi ya manukato

Swali: Makatazo ya kurudisha nyuma manukato yanapelekea kuwa ni haramu?

Jibu: Imekuja katika tamko jengine:

“Yayote anayepewa manukato basi asiyarudishe nyuma.”

Kuhusu hili ilikuwa ni katika mwendo wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba harudishi nyuma manukato. Kuhusu upokezi unaokataza kuyarudisha nyuma unahitaji kuangaliwa vyema. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza kuyarudisha nyuma.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24110/هل-النهي-عن-رد-الطيب-يقتضي-التحريم
  • Imechapishwa: 31/08/2024