Mabaki ya paka, punda na nyumbu

ar-Raajihiy: Vipi kuhusu mabaki ya nyumbu na punda?

Ibn Baaz: Si najisi kwa mujibu wa maoni sahihi. Ni kama mabaki ya paka, bali ni aula zaidi. Chakula kilichoachwa na paka kinaweza kuwa na uchafu zaidi. Ama mabaki ya punda na nyumbu hula kwenye lishe safi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameruhusu kula mabaki ya paka, licha ya kwamba wakati mwingine kukamata panya na vyenginevyo. Kwa hivyo mabaki ya nyumbu na punda yana haki zaidi kufaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24817/حكم-سور-البغل-والحمار
  • Imechapishwa: 13/12/2024