Swali: Ni nini maana ya wito kabla ya kuja Uislamu?
Jibu: Ni ubaguzi wa kikabila au wa ukoo. Huu ndio wito kabla ya kuja Uislamu. Ni kule kujivunia baba, babu, kabila, watu wa mji au desturi fulani. Mtu akaacha kufanya ubaguzi kwa ajili ya Qur-aan na Sunnah. Badala yake akafanya ubaguzi kwa ajili ya kabila, wazazi, watu wa mji wake au watu wengine.
Swali: Kuhusu makundi katika baadhi ya nchi kuna makundi yanayoshikamana na Qur-aan na Sunnah, lakini mara nyingine shaytwaan anawashinda ambapo wanakuwa na kiongozi, kisha wakagawanyika wakawa na viongozi wawili au watatu. Je, hili linahesabiwa kuwa ni kugawa umoja?
Jibu: Wanasihiwe na waelekezwe katika kheri ili wasitafunike umoja wao, bali wawe kitu kimoja. Yeyote anayefanya jambo kama hilo anatakiwa kushauriwa na kuelekezwa na ndugu zake na kuambiwa kwamba washikamane na Mkusanyiko na watafute suluhu kwa jambo linaloleta mtafaruku mpaka muafikiane wote.
Swali: Je, Hadiyth inawahusu watu wa namna hiyo?
Jibu: Ndiyo, ikiwa kuna ubaguzi au chuki baina yao. Lakini kama wanakubaliana katika maana moja, ingawa hawa wana shughuli zao na wale wana zao, kama kufundisha au kufanya kazi tofauti, lakini wanashirikiana na hawajagawanyika, basi Hadiyth hiyo haiwahusu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31151/ما-معنى-دعوى-الجاهلية-في-الحديث
- Imechapishwa: 08/10/2025
Swali: Ni nini maana ya wito kabla ya kuja Uislamu?
Jibu: Ni ubaguzi wa kikabila au wa ukoo. Huu ndio wito kabla ya kuja Uislamu. Ni kule kujivunia baba, babu, kabila, watu wa mji au desturi fulani. Mtu akaacha kufanya ubaguzi kwa ajili ya Qur-aan na Sunnah. Badala yake akafanya ubaguzi kwa ajili ya kabila, wazazi, watu wa mji wake au watu wengine.
Swali: Kuhusu makundi katika baadhi ya nchi kuna makundi yanayoshikamana na Qur-aan na Sunnah, lakini mara nyingine shaytwaan anawashinda ambapo wanakuwa na kiongozi, kisha wakagawanyika wakawa na viongozi wawili au watatu. Je, hili linahesabiwa kuwa ni kugawa umoja?
Jibu: Wanasihiwe na waelekezwe katika kheri ili wasitafunike umoja wao, bali wawe kitu kimoja. Yeyote anayefanya jambo kama hilo anatakiwa kushauriwa na kuelekezwa na ndugu zake na kuambiwa kwamba washikamane na Mkusanyiko na watafute suluhu kwa jambo linaloleta mtafaruku mpaka muafikiane wote.
Swali: Je, Hadiyth inawahusu watu wa namna hiyo?
Jibu: Ndiyo, ikiwa kuna ubaguzi au chuki baina yao. Lakini kama wanakubaliana katika maana moja, ingawa hawa wana shughuli zao na wale wana zao, kama kufundisha au kufanya kazi tofauti, lakini wanashirikiana na hawajagawanyika, basi Hadiyth hiyo haiwahusu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31151/ما-معنى-دعوى-الجاهلية-في-الحديث
Imechapishwa: 08/10/2025
https://firqatunnajia.com/maana-ya-wito-wa-kabla-ya-kuja-uislamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket