Maana ya pambo la muumini lililotajwa katika Hadiyth

Swali: Nini maana ya pambo la muumini?

Jibu: Pambo la muumini Peponi. Abu Hurayrah alifanya hivo ili ajizidishie pambo. Hadiyth inasema:

“Pambo la muumini litafika pale unapoishilia wudhuu´ wake.”[1]

Akawa anazidisha ili pambo lake lichukue nafasi kubwa. Hata hivyo hili halifahamishi kuwa kuzidisha kumewekwa katika Shari´ah. Pampo litaishilia pale mtu anapotia wudhuu´ mpaka juu kidogo ya viwiko vya mikono.

[1] Muslim (250).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24119/معنى-حلية-المومن-المذكورة-في-الحديث
  • Imechapishwa: 02/09/2024