Maana Ya Kwamba Sifa Za Allaah Ni Kamilifu

Swali: Tunasema kuwa Sifa za Allaah ni za milele. Nini maana yake?

Jibu: Maana yake ni kwamba hazina mwanzo. Allaah Hakupata Sifa ambayo hakuwa nayo hapo kabla. Tukisema kuwa imekuja hivi sasa, hii ina maana ya kwamba Allaah Alikuwa mpungufu kabla ya kutokea kwake. Namna hii ndivo wanavosema Jahmiyyah. Hii ina maana ya kwamba Alikuwa mpungufu. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ni mkamilifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331123.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015