Swali: Baadhi ya wafasiri wanasema katika tafsiri ya maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ
“Basi kumbusha ikiwa kunafaa ukumbusho.”[1]
kwamba maana yake ni kuwa kumbusha pale ambapo ukumbusho unanufaisha?
Jibu: Hili si sharti, bali ni sifa ya wingi wa hali. Kwa maana nyingine ni kwamba wajibu na ulazima huwa mkubwa zaidi pale watu wanaponufaika na ukumbusho. Kimsingi ni amri ya kukumbusha, huenda wakafaidika. Na kwa ajili hii imekuja katika Aayah nyingine:
فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ
”Basi kumbusha! Hakika mambo yalivyo wewe ni mkumbushaji tu.”[2]
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ
“Na kumbusha, kwani hakika ukumbusho [mawaidha] unawafaa Waumini.”[3]
Kwa hiyo mtu anatakiwa kukumbusha. Manufaa yako mikononi mwa Allaah. Lakini ikiwa ukumbusho unaleta manufaa, basi ulazima unakuwa mkubwa zaidi na faida huwa kubwa zaidi. Hivyo akiona kuna manufaa na faida, basi wajibu wake huzidi, huimarika na hukua.
[1] 87:09
[2] 88:21
[3] 51:55
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30050/ما-معنى-قوله-تعالى-فذكر-ان-نفعت-الذكرى
- Imechapishwa: 05/09/2025
Swali: Baadhi ya wafasiri wanasema katika tafsiri ya maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ
“Basi kumbusha ikiwa kunafaa ukumbusho.”[1]
kwamba maana yake ni kuwa kumbusha pale ambapo ukumbusho unanufaisha?
Jibu: Hili si sharti, bali ni sifa ya wingi wa hali. Kwa maana nyingine ni kwamba wajibu na ulazima huwa mkubwa zaidi pale watu wanaponufaika na ukumbusho. Kimsingi ni amri ya kukumbusha, huenda wakafaidika. Na kwa ajili hii imekuja katika Aayah nyingine:
فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ
”Basi kumbusha! Hakika mambo yalivyo wewe ni mkumbushaji tu.”[2]
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ
“Na kumbusha, kwani hakika ukumbusho [mawaidha] unawafaa Waumini.”[3]
Kwa hiyo mtu anatakiwa kukumbusha. Manufaa yako mikononi mwa Allaah. Lakini ikiwa ukumbusho unaleta manufaa, basi ulazima unakuwa mkubwa zaidi na faida huwa kubwa zaidi. Hivyo akiona kuna manufaa na faida, basi wajibu wake huzidi, huimarika na hukua.
[1] 87:09
[2] 88:21
[3] 51:55
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30050/ما-معنى-قوله-تعالى-فذكر-ان-نفعت-الذكرى
Imechapishwa: 05/09/2025
https://firqatunnajia.com/maana-sahihi-ya-kumbusha-ikiwa-kunafaa-ukumbusho/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket