Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sijaacha mtihani wenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake. Mtihaniwa kwanza kwa wana wa israaiyl ilikuwa juu ya wanawake.”[1]

Kwa ajili hii maadui zetu ambao ni maadui wa Uislamu, bali ni maadui wa Allaah na Mtume Wake, ambao ni mayahudi, manaswara, washiriina, wakomunisti, vijukuu vyao, mikia yao na wafuasi wao, wote hawa wanatumia juhudi kubwa kuwafitinisha waislamu kwa kuwatumia wanawake. Wanaita mwanamke kuonyesha mapambo yake, mwanamke kuchanganyika na mwanaume na tabia mbaya. Wanafanya hayo kwa ndimi zao, uandishi na matendo yao. Wanajua kuwa fitina kubwa ambayo itamfanya mwanadamu kumsahau Mola Wake na dini yake ni kwa kumtumia mwanamke.

[1] al-Bukhaariy (5096)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/95)
  • Imechapishwa: 01/02/2023