Swali: Nilinunua kipande cha ardhi kutoka kwa mwenyewe kwa malipo ya awamu kwa muda wa miaka minne kwa kiasi fulani cha fedha. Baada ya takriban mwaka mmoja nilikubaliana naye kwamba nimlipe awamu zote zilizobaki kwa mkupuo mmoja kwa sharti anipunguzie kiasi tulichokubaliana. Ni yepi maoni yenu kuhusu hili? Je, zakaah yake inaanza tangu kununua au baada ya kuandikishwa rasmi kwangu?

Jibu: Suala hili lina maoni tofauti baina ya wanazuoni. Ni suala la “Punguza na ulipie mapema”, nalo linajulikana kwa wanazuoni. Imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaambia Banuu an-Nadhwiyr alipokusudia kuwahamisha na wakalalamika kwamba wana madeni kwa watu, akasema:

”Punguzeni na lipeni mapema.”

Kwa hiyo lililo sahihi ni kwamba inajuzu. Ikiwa mdaiwa atasema kuwa yeye analipa haki yake kwa mkupuo mmoja, lakini akamuomba apunguze. Kwa mfano deni ni 4,000 kwa miaka minne, akasema kuwa atalipa pesa yote sasa ikiwa atampunguzia 1,000. Mwenye deni akakubali kwamba amletee 3,000 na kwamba atamsamehe 1,000. Hakuna ubaya katika hilo. Lililo sahihi ni kwamba inajuzu, japokuwa wanazuoni wengi wanaona kinyume chake. Lakini sahihi ni kwamba inajuzu, kwa sababu ndani yake kuna maslahi ya kuharakisha haki na kuondoka kwa dhimmah. Ndani yake kuna maslahi mawili: kuharakisha haki kwa mwenyewe hata kama imepungua badala ya kusubiri miaka, anapewa mara moja. Kumpunguzia mdaiwa sehemu ya deni. Lililo sahihi katika hili ni kwamba inajuzu. Hili ni suala la ”Punguzeni na lipeni mapema”. Unakuwa na haki kwa Zayd 1,0000 SAR zitakazotimia Ramadhaan ijayo, ukamuomba kuwa utamlipa 8,000 na akusamehe sehemu iliyobaki. Ikiwa amekupa 800 na akakusamehe 200 kwa sababu ya kulipa mapema, hakuna ubaya. Vivyo hivyo kwa yaliyo mengi au machache.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3396/بيان-الراجح-في-مسالة-ضع-وتعجل
  • Imechapishwa: 14/09/2026