123 – Muhammad bin ´Abdil-A´laa ametukhabarisha: al-Mu´tamir (bin Sulaymaan) ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye ameeleza:
”Wakati Aayah isemayo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ
“Enyi walioamini! Msizinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Mtume na wala msiseme naye kwa sauti ya juu kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, yasije yakaporomoka matendo yenu nanyi hamhisi.”[1]
ilipoteremshwa, Thaabit bin Qays alisema: “Naapa kwa Allaah! Ni mimi ndiye nilikuwa napaza sauti mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ninaogopa kuwa Allaah amenighadhibikia.” Kwa hiyo akahuzunika na kubaki nyumbani. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipomkosa, akamuulizia. Akaambiwa: “Ee Mtume wa Allaah! Anasema `Nachelea kuwa mimi ni miongoni mwa watu wa Motoni; mimi nilikuwa nikipaza sauti yangu mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)`.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Bali yeye ni katika watu wa Peponi.” Tulikuwa tukimuona akitembea kati yetu – mtu katika watu wa Peponi.”[2]
124 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Khaalid ametukhabarisha: Humayd ametukhabarisha, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza:
“Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowasili Madiynah, Thaabit bin Qays alitoa neno na kusema: “Tutakulinda na yale tunayojilinda sisi wenyewe na watoto wetu. Nini tututachopata?” Akasema: ”Pepo.” Akasema: “Tumeridhika.”[3]
[1] 49:02
[2] al-Bukhaariy (3613) na Muslim (187).
[3] al-Haakim (3/234), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 90
- Imechapishwa: 14/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 90
Imechapishwa: 14/09/2026
https://firqatunnajia.com/fadhilah-za-thaabit-bin-qays/