Swali: Je, kuhesabu muda uliopangwa unaanza mwanzoni mwa kupangusa au mwanzoni mwa kutawadha?

Jibu: Hapana, baada ya kupata hadathi. Muda wa kupangusa unaanza kuhesabiwa baada ya kuchenguka wudhuu´. Kwa mfano kama alizivaa wakati wa ´Aswr na ukachenguka wudhuu´ wake baada ya ´Ishaa, muda unaanze kuhesabiwa baada ya ´Ishaa. Kwa msemo mwingine hatohesabu ule muda wa ´Aswr, Magharib na ´Ishaa. Muda wa kupangusa ni mchana mmoja na usiku wake baada ya kupangusa na michana mitatu na nyusiku zake baada ya kupangusa, nikikusudia kuhesabu kuanzia baada ya kuchenguka wudhuu´ wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24739/متى-يبدا-التوقيت-في-المسح-على-الخفين
  • Imechapishwa: 05/12/2024