Lini inaanza na lini inamalizika I´tikaaf?

Swali: Kama mtu anataka kukaa I´tikaaf msikitini katika zile siku kumi zote za mwisho za Ramadhaan – ni lini ataanza kuingia msikitini? Ni lini inamalizika I´tikaaf yake?

Jibu: al-Bukhaariy na Muslim (Rahimahumu Allaah) wamepokea kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapotaka kukaa I´tikaaf basi anaswali Fajr kisha anaingia ndani ya I´tikaaf yake.”

Muda wa I´tikaaf yake zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan inamalizika kwa kuzama kwa jua ile siku yake ya mwisho.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaBySubjects.aspx?cultStr=ar&View=Page&HajjEntryID=0&HajjEntryName=&RamadanEntryID=0&RamadanEntryName=&NodeID=1396&PageID=3802&SectionID=3&SubjectPageTitlesID=25234&MarkIndex=1&0#%d8%a5%d8%b0%d8%a7%d8%a3%d8%b1%d8%a7%d8%af%d8%b4%d8%ae%d8%b5%d8%a3%d9%86%d9%8a%d8%b9%d8%aa%d9%83%d9%81%d9%81%d9%8a%d8%a7%d9%84%d8%b9%d8%b4%d8%b1
  • Imechapishwa: 23/04/2022