Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema:

“Katika zama hizi hakuna wanachuoni?”

Je, wanachuoni wataendelea kuwepo mpaka siku ya Qiyaamah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu wakiwa juu ya haki hali ya kushinda, hawatowadhuru wenye kuwapinga wala wenye kuwakosesha nusura mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).”

Kisha huyu anasema kuwa hakuna?!

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14819
  • Imechapishwa: 28/06/2020