“Leo hakuna haja ya Zakaat-ul-Fitwr kwa kuwa hakuna mafukara”

Swali: Ni ipi hukumu ya msemo huu:

“Hakuna haja ya kutoa Zakaat-ul-Fitwr leo, kwa kuwa hakuna mafukara”?

Jibu: Ndio, kwa kuwa yeye ni tajiri anafikiria watu wote ni kama yeye! Haya ni maneno ya kipuuzi na haijuzu kusema hivi. Ina maana iachwe faradhi miongoni mwa faradhi za Kiislamu na kusema hakuna mafukara?!! Kuna mafukara wengi. Huenda anataka wote waje kujitambulisha na kujijulisha kwake!

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-1-24.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014