Kumpa zakaah mtu ambaye unafikiria ataitumia katika haramu

Swali: Akiniomba mwenye kuomba na nikawa na dhana kubwa ya kwamba ananunua vitu vya haramu, kama sigara na kadhalika. Je, dhana yangu hii kubwa inatosheleza kutompa (Zakaah)?

Jibu: Ndio. Dhana kubwa inaenda katika manzilah ya yakini. Hii ni kanuni. Ukiwa na dhana kubwa ya kwamba ananunua vitu vya haramu, usimpe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-1-24.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014