Lazima unachofanyia Tayammum kiwe na udongo au vumbi

Swali: Wanazuoni wameweka masharti ya kwamba ni lazima kuwa na vumbi katika udongo [wa Tayammum]

Jibu: Kama alivosema Allaah (‘Azza wa Jall):

فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

“..abasi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu kutoka humo.”[1]

Maana ya ´kutoka humo` ni kile kinachotokana nao tu kwa kuwepo udongo au kuwepo vumbi. Aidha udongo au vumbi.

[1] 05:06

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27522/هل-يشترط-وجود-الغبار-في-تراب-التيمم
  • Imechapishwa: 11/04/2025