Kwenda makaburini kuwaswalia maiti kila alhamisi na ijumaa

Swali: Baadhi ya wasiokuwa wasomi wanaingia makaburini siku ya alhamisi na wanamswalia kila maiti aliyekufa katika siku hii na wako wengine wanawaswalia baba zao kila ijumaa. Unasemaje juu ya kitendo hichi?

Jibu: Maoni yangu ni kuwa swalah hii ni Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiyatembelea makaburi na wala hayaswalii. Bali alikuwa akiwaombea du´aa iliyowekwa katika Shari´ah:

السَّلامُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الدِّيَارِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُسْلِمِين وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللهُ بكم لاحِقُونَ نَسْأَلُ الله لَنَا وَلَكُمْ الْعَافِية

“Amani ya Allaah iwe juu yenu manyumba ya wakazi waumini. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana nanyi. Allaah awarehemu wenye kutangulia katika sisi na nyinyi na wataokuja nyuma. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi afya.”[1]

اللهم لا تحرمنا أجره ولا تفتنـا بعـده و اغفر لنا و له

“Ee Allaah! Usitunyime ujira wao na wala usitujaribu baada yake. Utusamehe sisi na wao.”[2]

Kuhusu kuwaswalia swalah ya jeneza ni Bid´ah. Ni wajibu kulikemea hilo na kuwabainishia wale wenye kulifanya kuwa haliwakurubishi mbele ya Allaah, kwa kuwa ni Bid´ah. Isitoshe hayamnufaishi kitu maiti, kwa kuwa ni Bid´ah.

[1] Muslim (974).

[2] Ahmad (4/79), Abuu Daawuud (3201) na Ibn Maajah (1498).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/145)
  • Imechapishwa: 15/09/2021