Inafaa kujenga msikiti makaburini kwa ajili ya wenye kumswalia maiti?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka bomba la maji au kujenga msikiti makaburini kwa wale ambao hawakumswalia maiti?

Jibu: Ni sawa kuweka bomba la maji makaburini au pembezoni mwake.

Kuhusu kujenga msikiti makaburini haijuzu. Hata hivyo ni sawa kutenga mahali pa kuswalia (صلى) karibu na bomba hilo kwa njia ya kwamba ni pahala pa kuswalia swalah ya jeneza tu na hakuswaliwi zile swalah tano. Kitendo kama hichi hakina neno60.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/144)
  • Imechapishwa: 15/09/2021