Kwenda kwa mchawi kuhakikisha kama amerogwa

Swali: Je, inafaa kwa mtu kwenda kwa mchawi kujua kama amerogwa au hakurogwa?

Jibu: Haijuzu. Ni haramu kuwasadikisha wachawi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayemwendea mpiga ramli au kuhani akamsadikisha kwa aliyoyasema, basi hakika ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Wachawi hawasadikishwi, hawaendewi wala kuwaheshimishwi. Ni lazima kuwashtaki. Ambaye atajulikana kuwa ni mchawi anatakiwa kuambiwa kutubia. Vinginevyo atauliwa[1]. Kwa sababu ni mtu muovu kabisa na anakula mali za watu pasi na haki. Hawaaminiwi.

[1] Nani mwenye haki ya kuwaua Khawaarij? – al-Firqah an-Naajiyah (firqatunnajia.com)

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-26-12-1435هـ
  • Imechapishwa: 19/06/2022