Kwenda Hajj zaidi ya mara moja kwa aliye na deni

Swali: Je, inafaa kwa mwanaume kumpeleka mama yake kuhiji ambaye bado hajahiji, hali akiwa ana deni analolipa kwa mafungu ya kila mwezi na muda wa kulilipa bado haujafika? Je, deni hili linahesabiwa kuwa kizuizi cha kwenda Hajj, khaswa kwa kuwa yeye tayari ameshatekeleza Hajj ya faradhi?

Jibu: Ikiwa ameshatekeleza Hajj ya faradhi, basi anapaswa kulipa deni. Ikiwa anaweza kulipa mafungu hayo kwa wakati wake na Hajj haitamuathiri katika kulipa deni hilo, basi hakuna tatizo kumpeleka mama yake Hajj. Hili ni katika kumfanyia wema, kwa sababu si wajibu kwake kufanya hivyo. Ama ikiwa hawezi kulipa deni hilo au muda wa kulilipa umefika, basi asimpeleke kwa sababu deni linatangulizwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 26/09/2026