Swali: Kuna mtu mwenye umri wa miaka kumi na minane alifungua swawm ya Ramadhaan siku moja. Udhuru wake ulikuwa kwamba alichoka kwa sababu hakula daku. Kisha akaikidhi siku hiyo baada ya Ramadhaan. Huenda kufungua kwake kulikuwa kwa sababu ya kutojua hukumu ya kufungua katika mwezi wa Ramadhaan. Kisha mtu huyo akafariki baada ya mwezi wa Ramadhaan, hali akiwa ameshalipa swawm ya siku hiyo. Je, kuna jambo lolote linalomlazimu mmoja wa watu wa familia yake kulifanya kwa niaba yake?
Jibu: Kwa kuwa alilipa, basi himdi zote ni za Allaah. Atakuwaje hajui hali ya kuwa anaishi miongoni mwa waislamu?! Lakini tukikadiria kwamba alilazimika na akaogopa kufa, basi hakuna tatizo kwake kufungua swawm ikiwa anaogopa kuangamia. Kwa mfano, ikiwa kiu itamzidia sana hali akiwa amefunga, basi anakunywa kiasi cha kujiokoa, kisha anailipa siku hiyo. Vivyo hivyo ikiwa njaa itamzidia sana na akaogopa kufa, basi anaweza kula, kama mtu aliyelazimika kula mnyama aliyekufa. Sidhani kwamba kijana huyu hali yake ilifikia kiwango hicho. Kinachokusudiwa ni kwamba ikiwa aliikidhi siku hiyo, basi huenda hilo likamtosheleza – Allaah akitaka.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 26/09/2026
Swali: Kuna mtu mwenye umri wa miaka kumi na minane alifungua swawm ya Ramadhaan siku moja. Udhuru wake ulikuwa kwamba alichoka kwa sababu hakula daku. Kisha akaikidhi siku hiyo baada ya Ramadhaan. Huenda kufungua kwake kulikuwa kwa sababu ya kutojua hukumu ya kufungua katika mwezi wa Ramadhaan. Kisha mtu huyo akafariki baada ya mwezi wa Ramadhaan, hali akiwa ameshalipa swawm ya siku hiyo. Je, kuna jambo lolote linalomlazimu mmoja wa watu wa familia yake kulifanya kwa niaba yake?
Jibu: Kwa kuwa alilipa, basi himdi zote ni za Allaah. Atakuwaje hajui hali ya kuwa anaishi miongoni mwa waislamu?! Lakini tukikadiria kwamba alilazimika na akaogopa kufa, basi hakuna tatizo kwake kufungua swawm ikiwa anaogopa kuangamia. Kwa mfano, ikiwa kiu itamzidia sana hali akiwa amefunga, basi anakunywa kiasi cha kujiokoa, kisha anailipa siku hiyo. Vivyo hivyo ikiwa njaa itamzidia sana na akaogopa kufa, basi anaweza kula, kama mtu aliyelazimika kula mnyama aliyekufa. Sidhani kwamba kijana huyu hali yake ilifikia kiwango hicho. Kinachokusudiwa ni kwamba ikiwa aliikidhi siku hiyo, basi huenda hilo likamtosheleza – Allaah akitaka.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 26/09/2026
https://firqatunnajia.com/kijana-amefungua-swawm-ya-ramadhaan-kwa-sababu-ya-machovu-makali/