Matangazo ya kampeni za Hajj msikitini

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayesambaza matangazo ya kampeni za Hajj msikitini?

Jibu: Ikiwa msambazaji anapewa ujira, kwa maana kwamba lengo lake limekuwa ni kupata fedha, basi hili halijuzu. Ama ikiwa hakuna ujira katika kampeni hizo za Hajj, basi hakuna tatizo kwa sababu hii ni kuwaalika watu kwenye ´Ibaadah. Lakini ikiwa lengo lake ni kupata fedha, basi haijuzu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 26/09/2026