Kwanini asikufurishwi anayepinga sifa za Allaah?

Swali: Je, anakufuru yule mwenye kukanusha baadhi ya sifa za Allaah au zote?

Jibu: Kunahitajia upambanuzi. Anatakiwa kusimamishiwa hoja. Anaweza kuwa hajui baadhi ya sifa. Anatakiwa kubainishiwa yale yaliyothibiti katika Qur-aan na Sunnah. Akikanusha Mwingi wa huruma (ar-Rahmaan), Mwenye hekima (al-Hakiym), Mtakasifu (al-Qudduus) au mfalme (al-Malik) anakufuru. Akiwa si msomi anatakiwa kubainishiwa yale yaliyokuja katika Qur-aan na Sunnah Swahiyh.

Swali: Vipi ikiwa anapindisha ile maana yake?

Jibu: Kupindisha maana kunatofautiana. Ni kama mfano wa Ashaa´irah na wengineo. Kuna wanaowakufurisha na kuna ambao hawawakufurishi. Katika kupindisha maana (Ta´wiyl) kuna utata. Ni tofauti na Mu´tazilah na Jahmiyyah ambao ni makafiri. Kwa kuwa hawa wamekanusha sifa za Allaah zote na majina.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 102
  • Imechapishwa: 05/01/2017