Ingelikuwa vizuri kama utasoma kitabu  ”ar-Radd ´alaa As-ilat-ith-Thawrah” cha Shaykh na Dr. Fahd al-Fuhayd. Kwa sababu wakati mwingine mtunzi wa As-ilat-ith-Thawrah anasema mambo yanayofanana na kufuru. Sisemi kuwa anakufuru; pengine hajui kile anachokisema. Humo ameandika:

“Raia wakitaka kuchagua dini nyingine au uongozi mwingine usiokuwa Uislamu basi ni wajibu kupitisha chaguo la raia.”

Mnasemaje juu ya hilo? Kama isingelikuwa uchaji basi tungelimkufurisha. Lakini pengine hakuwa na fahamu wakati alipoandika jambo hilo kama ambavo hakuwa na fahamu katika matukio mengi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148562
  • Imechapishwa: 16/08/2023