Swali: Akiniomba mzushi kwenda katika msikiti wao kuwatolea mawaidha na Khutbah, nende au nikatae?

Jibu: Usikatae endapo Ahl-ul-Bid´ah watakuomba kwenda katika msikiti wao kwa ajili ya kuwatolea Khutbah, mawaidha au semina au muhadara. Lakini unalazimika kuzungumzia zile Bid´ah walizonazo. Zitahadharishe na bainisha madhara yake kwa dalili za Qur-aan na Hadiyth. Pengine Allaah kupitia kalima, mawaidha au Khutbah akamwongoza wa kumwongoza. Hivyo ukalipwa thawabu kwa jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=tsr2zBvUy0Y
  • Imechapishwa: 16/08/2023