Swali: Je, kufuru ya mtu ambaye anarudisha Hadiyth ya mpokezi mmoja (Hadiyth-ul-Aahaad) na asiitumie kama hoja katika mambo ya ´Aqiydah inamtoa katika dini?

Jibu: Hii ni ´Aqiydah ya Mu´tazilah na wafuasi wao katika wanafalsafa leo. Wanaitwa wanafalsafa kwa kuwa wanategemea akili. Huyu ni mpotevu na amekosea. Ikijua fika kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kitu hichi, pamoja na hivyo akasema “hata kama Mtume atakuwa amesema” – kama wanavosema baadhi ya waandishi – huyu anakufuru kwa sababu anamkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama ikiwa haikuthibiti kwake usahihi wa isnadi, huyu anapewa udhuru kwa ujinga wake. Wanachuoni wengine wametambua usahihi wa isnadi na huyu hakuutambua hivyo anapewa udhuru kwa ujinga wake. Ama lau atajua usahihi wa isnadi na akasema “hata kama Mtume atakuwa amesema”… Kwa kuwa baadhi yao wanasema kuwa hawaitendei kazi kwa kuwa inaenda kinyume na akili. Haijalishi kitu hata kama Mtume amesema hivo kwa kuwa inaenda kinyume na akili, huyu ni kafiri bila ya shaka kwa sababu anamkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_08.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2015