Swali: Nini maana ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Pengine wakakhafifishiwa adhabu midhali bado [makuti hayo] ni kijani.”[1]?

Jibu: Kutokana na hekima kubwa ya kwamba makuti hayo mawili yanamfaa muda wa kuwa yana unyevunyevu. Baadhi ya Salaf wamesema ya kwamba inamtukuza Allaah. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita karibu na makaburi mawili na akasema: “Hakika wawili hawa wanaadhibiwa na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Lakini hata hivyo ni jambo kubwa. Kuhusu mmoja wao alikuwa akitembea na kueneza umbea na mwengine alikuwa hajichungi na mkojo wake.” (al-Bukhaariy (218) na Muslim (292).)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24148/معنى-حديث-لعله-يخفف-عنهما-ما-لم-ييبسا
  • Imechapishwa: 07/09/2024