Swali: Ndugu yake maiti, wakati anapomtembelea makaburini, inafaa kwake kukaa na kumweleza yanayoendelea juu yake na familia yake?

Jibu: Hapana. Amsalimie, amwombee du´aa, ni mamoja kwa kuketi chini au kwa kusimama, kisha aondoke zake. Ama kumweleza wanayofanya familia yake na kumpasha khabari na mfano wa hayo, haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 02/06/2023