Kuzugumzia magomvi na fitina iliyotokea kati ya Maswahabah

Kuzungumzia fitina iliyopitika kati ya Maswahabah hakutuzidishii chochote zaidi ya upotevu. Kwa sababu katika hali hii itapelekea kuwaponda baadhi ya Maswahabah na kupetuka mipaka kwa wengine kama walivofanya Raafidhwah. Walipopetuka mipaka kwa Ahl-ul-Bayt wakadai kuwa ni kuwapenda. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba watu wa familia ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wenye kujitenga mbali kabisa na kupindukia kwao. Mtu wa kwanza aliyejitenga na upindukiaji wao ni ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).

Saba´iyyah ambao ni wafuasi wa ´Abdullaah bin Sabaa´ – na yeye ndiye wa kwanza kuzusha madhehebu ya Raafidhwah katika Ummah huu na alikuwa ni myahudi aliyedhihirisha Uislamu ili aubomoe Uislamu kama alivosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ambaye alizisoma hali za watu na kuzijua. Amesema kuwa ´Abdullaah bin Sabaa´ ni myahudi aliyeingia katika Uislamu kwa lengo la kuubomoa kama alivyoingia Buulis katika dini ya kinaswara ili aweze kuubomoa. ´Abdullaah bin Sabaa´ – Allaah amlipe anachokistahiki – alidhihirisha kuwa anawapenda watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam), kwamba anawatetea na ´Aliy bin Abiy Twaalib. Akapetuka mipaka mpaka akafikia kusema kumwambia ´Aliy bin Abiy Twaalib “Wewe ndiye Allaah wa haki.” Allaah amlaani. ´Aliy bin Abiy Twaalib akaamrisha kukongwe moto na baada ya hapo akawaita watu hawa na wafuasi wake na kuwatupa ndani ya moto. Tazama alivowaunguza kwa moto kwa sababu dhambi yao ilikuwa kubwa. Inasemekana vilevile kuwa ´Abdullaah bin Sabaa´ alikwepa na kukimbia kwenda Misri. Allaah ndiye Anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/279-280)
  • Imechapishwa: 21/10/2024