Baadhi ya watu wanafikiria kuwa sio wajibu kumtii mtawala isipokuwa tu katika yale ambayo Allaah ameamrisha. Hili ni kosa. Kwa sababu yale ambayo Allaah ameamrisha ni wajibu kuyafanya na kujisalimisha nayo, haijalishi kitu sawa ikiwa mtawala ametuamrisha nayo au hakutuamrisha nayo. Kuna hali tatu:
1 – Anayoamrisha mtawala yawe yameamrishwa Kishari´ah, kwa mfano anaamrisha kuswali kwa mkusanyiko, hapa ni wajibu kufanya aliyoamrisha kwa sababu yameamrishwa na Allaah, Mtume Wake na mtawala.
2 – Mtawala akaamrisha kumuasi Allaah; kama kuacha jambo la wajibu au kufanya jambo la haramu, hapa hatiiwi wala hasikizwi.
3 – Mtawala akawaamrisha watu jambo ambalo sio amri wala sio maasi kwa mujibu wa Shari´ah, hapa ni wajibu kumtii. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]
Kumtii mtawala katika mambo yasiyokuwa maasi, ni sehemu katika kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 04:59
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/278-279)
- Imechapishwa: 21/10/2024
Baadhi ya watu wanafikiria kuwa sio wajibu kumtii mtawala isipokuwa tu katika yale ambayo Allaah ameamrisha. Hili ni kosa. Kwa sababu yale ambayo Allaah ameamrisha ni wajibu kuyafanya na kujisalimisha nayo, haijalishi kitu sawa ikiwa mtawala ametuamrisha nayo au hakutuamrisha nayo. Kuna hali tatu:
1 – Anayoamrisha mtawala yawe yameamrishwa Kishari´ah, kwa mfano anaamrisha kuswali kwa mkusanyiko, hapa ni wajibu kufanya aliyoamrisha kwa sababu yameamrishwa na Allaah, Mtume Wake na mtawala.
2 – Mtawala akaamrisha kumuasi Allaah; kama kuacha jambo la wajibu au kufanya jambo la haramu, hapa hatiiwi wala hasikizwi.
3 – Mtawala akawaamrisha watu jambo ambalo sio amri wala sio maasi kwa mujibu wa Shari´ah, hapa ni wajibu kumtii. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]
Kumtii mtawala katika mambo yasiyokuwa maasi, ni sehemu katika kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 04:59
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/278-279)
Imechapishwa: 21/10/2024
https://firqatunnajia.com/hali-tatu-za-kumtii-mtawala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)