Kuzidisha “na baraka Zake” wakati wa Tasliym

Swali: Je, anapomaliza mswaliji kutoka katika swalah yake na akatao kutoa salamu aseme:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

kuliani na kushotoni au aseme:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

peke yake? Ni ipi hukumu ya swalah ya ambaye amefanya hivo kwa kuzidisha:

وبركاته

‘“… na baraka Zake.“?

Jibu: Kilichohifadhiwa katika Sunnah ni kusema:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

peke yake. Hiki ndicho kilichowekwa katika Shari´ah aseme:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

kuliani mwake na kushotoni mwake. Nyongeza inayosema:

وبركاته

‘“… na baraka Zake.”

ni jambo lenye makinzano kwa wanazuoni. ´Alqamah bin Waail amesimulia kutoka kwa baba yake ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema ifuatavyo:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

Lakini wanazuoni wamekinzana kama imesihi au haikusihi ´Alqamah kusikia kutoka kwa baba yake. Wengine wamesema kuwa kuwa cheni ya wapokezi wake imekatika. Kilichowekwa katika Shari´ah kwa muumini ni yeye asizidishe na akomeke katika:

ورحمة الله

“.. na rehema za Allaah.”

Atakayezidisha kwa kufikiri kuwa imesihi au kwa kutokojua hukumu basi swalah yake ni sahihi. Lakini bora na lililo salama zaidi ni yeye asizidishe kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano ya wanazuoni na jengine kwa ajili ya kutendea kazi amri iliyothibiti na kwa ajili ya kuchukua tahadhari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4113/حكم-زيادة-وبركاته-في-تسليم-الصلاة
  • Imechapishwa: 25/10/2021