Kuzawadiana vitu ambavyo vinaweza kutumiwa katika kheri na shari

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa zawadi baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutumiwa katika kheri na shari kama mfano wa mikanda na kadhalika?

Jibu: Ukimpa zawadi mtu ambaye atavitumia katika kheri ni sawa. Ukimpa zawadi mtu ambaye atavitumia katika kheri vinakuwa ni vyenye kumsaidia katika kheri na kushirikiana katika wema na uchaji Allaah. Na ukimpa zawadi mtu ambaye unajua atavitumia katika shari unakuwa ni mwenye kushirikiana naye katika madhambi. Usimpe zawadi isipokuwa tu yule unayejua kuwa atavitumia katika kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 01/05/2015