Kuyaabudia makaburi kwa kuyazunguka

Swali: Ni ipi hukumu ya yale yanayotokea kwa waislamu wengi katika baadhi ya miji ambapo wanatufu makaburi na wanajikurubisha kwayo kwa madai kwamba hawayaabudu na kwamba wanafanya Tawassul kwayo mbele ya Allaah? Ni vipi wanaraddiwa watu hawa?

Jibu: Hii kwa dhati yake ndio shirki ya washirikina; shirki ya Quraysh, shirki ya watu wa Nuuh, watu wa Huud, watu wa Swaalih na watu wa Ibraahiym. Walikuwa wenye kudai kwamba wanawaabudia kwa ajili ya maombezi na njia. Tunawaambia kwamba kitendo hicho ni batili. Allaah hakuwafanya watu hao kuwa ni njia. Allaah amefanya njia ya kuweza kumfikia ni kule kumtii, kumwomba du´aa na kumtakasia Yeye nia. Hakufanya kumshirikisha na kuwaabudu wengine asiyekuwa Yeye ni njia ya kuweza kumfikia. Unapomwabudu mwengine asiyekuwa Yeye na ukamwomba mwengine asiyekuwa Yeye umemjaalia Allaah mshirika na mwenza. Kitendo hichi hakistahiki. Kwa sababu viumbe wameumbwa kwa ajili ya kumwabudu na Mitume wametumilizwa ili kuwalingania viumbe kumfasiria ´ibaadah Allaah na Allaah asiwe na mshirika katika chochote katika hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-الطواف-حول-القبور-والأضرحة-والتقرب-إليها
  • Imechapishwa: 11/06/2022