Swali: Nikiweka picha ya Shaykh kwenye simu ili niweze kumkumbuka na kumuombea rahmah, ni sahihi kwamba ni katika kupetuka mipaka na imekatazwa?

Jibu: Ndio. Usiweke picha. Picha haijuzu. Haijuzu kubeba picha wala kuihifadhi isipokuwa kwa dharurah, na jambo hili si dharurah. Hii si dharurah. Jambo hili linaweza kuwa ni kupindukia. Inatosha kwako kumuombea du´aa na kumuombea msamaha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (34) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid-17-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017