Swali: Katika matembezi yetu ya baadhi ya makaburi tuliona baadhi ya mambo kwenye makaburi ya waislamu ikiwa ni pamoja vilevile na kuweka kipande cha chuma usawa na kaburi kama alama ya kaburi hilo au chupa iliotupu. Baadhi ya watu wanaenda mbali zaidi katika kuweka alama ya kaburi kwa kiasi cha kwamba wanafikia kuandika juu ya kaburi jina la yule maiti na tarehe alifariki na kuandika hayo kwa aina ya kuchimba kwenye jiwe au mti wa mtende unaosimikwa ndani ya simenti na mfano wake. Je, mambo haya yanafaa?

Jibu: Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba yamechukizwa. Kwa sababu ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia Abul-Hayyaaj al-Asadiy:

“Hivi nisikutume juu ya kazi aliyonituma kwayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Usiache picha hata moja isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”

Mtu anaweza kuwaombea wafu hata akiwa nyumbani mwake. Haikushurutishwa mtu aende kwenye kaburi la mwingine. Yakionekana hayo kwenye makaburi basi wanatakiwa waambiwe wahusika wa nchi. Ni mamoja wahusika wa nchi hii au nyingine kwa lengo la kuyaondosha mambo haya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1416
  • Imechapishwa: 23/12/2019