Kumuwekea mswaliji Sutrah na kupiga msitari

Swali 17: Ni ipi hukumu ya kuweka Sutrah kwenye swalah pamoja na kunitajia dalili? Je, Hadiyth inayosema kuchora msitari katika Sutrah ni Swahiyh au hapana? Je, ni miongoni mwa Sunnah kumwekea Sutrah ambaye hakujiwekea?

Jibu: Kuhusu kuweka Sutrah maoni sahihi ni kwamba ni lazima. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ataposwali mmoja wenu basi aswali kwa kuelekea Sutrah na aisogelee.”

Kuhusu Hadiyth ya kupiga msitari ni dhaifu.

Ukimuona nduguyo anaswali pasi na kuweka Sutrah ambapo ukamuwekea ni jambo ambalo halina neno. Ni miongoni mwa kusaidiana katika mambo ya kheri na kufunza.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 23/12/2019