Swali: Ni ipi hukumu ya kugeuza msikiti ukumbi wa msikiti ukafanywa kilabu cha mazoezi kwa lengo la kuwavuta kutoka barabarani kuja msikitini?

Jibu: Hiki ni kitendo batili. Hii ina maana kwamba vijana wanakuja msikitini kwa lengo la kucheza. Ina maana kwamba wanakuja kwa sababu ya matamanio yao. Haitakiwi jambo hilo ndio liwavute kuja msikitini. Matumaini, woga na khofu ndio yanatakiwa kuwavuta kuja msikitini. Uchungaji na matahadharisho ndio ndio yanatakiwa kuwavuta kuja msikitini. Kwa mfano Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pepo imezingirwa na vya kuchukiza na Moto umezingirwa na matamanio.”

Kadhalika ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Dunia hiyo inatupa mgongo na Aakhirah hiyo inasogea yaja. Kila kimoja katika viwili hivyo kina watoto na kuweni ni katika watoto wa Aakhirah na msiwe ni katika watoto wa duniani. Kwani hakika hii leo ni matendo pasi na hesabu na kesho ni hesabu pasi na matendo.”

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Neema mbili zinawadanganya watu wengi: uzima na faragha.”

Wanatakiwa kupendezewa na kuogopeshwa. Ama kuwatengea maeneo fulani msikitini kwa sababu ya kuja kucheza ni kitendo kiovu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=78954&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 18/12/2020