Makusudio ya maneno haya ni kwamba mwandishi – Imaam al-Aajurriy – na Salaf-us-Swaalih wanaonelea kuwa kuwaua Khawaarij ni haki na mwenye kuwaua – sawa ikiwa ni ´Aliy au mtu mwingine – yuko katika haki. Kama tulivyotangulia kusema kwamba kuwaua ni haki mpaka siku ya Qiyaamah[1].

Kwa ajili hii wanachuoni na watu waheshimiwa katika Ummah huu walikuwa wakipigana bega kwa bega wakiwa pamoja na viongozi madhalimu, hata pamoja na al-Hajjaaj dhalimu na muharibifu, walikuwa wanaonelea kuwa yuko katika haki kwa kuwaua watu hawa.

Ahl-ul-Bid´ah ni shari na watu khatari. Mpaka hata Sallaam bin Abiy Mutwiy´ alikuwa ni katika wanachuoni bora wa Kuufah na mwenye bura zaidi katika wao. Anasema:

“Ninaapa kwa Allaah lau nitakutana na Allaah nikiwa na daftari la al-Hajjaal ni bora kwangu kuliko kukutana Naye nikiwa na daftari la ´Amr bin ´Ubayd.”

´Amr bin ´Ubayd ni mwenye kuipa nyongo dunia na mtawa, lakini hata hivyo ni mpotevu na mtu wa Bid´ah. al-Hajjaaj ni dhalimu na muuaji. Madaftari yote mawili ni meusi. Lakini daftari la ´Amr ni leusi zaidi na limejaa uchafu zaidi kuliko daftari la al-Hajjaaj. Huku ndio kuwa na uelewa [katika Dini] wa Salaf. Kwa ajili ndio maana unakuta kuna vitabu vingi visivyohesabika ambavyo vimewafedhehi, kuraddi upotevu, kubainisha shari, ´Aqiydah na khatari yao kwa Ummah.

Hii ndio manhaj ya Salaf ambayo watu wanatakiwa kuifahamu na wasimame kidete dhidi ya Ahl-ul-Bid´ah kwa msimamo kama huu sugu. Kwa kuwa Bid´ah inaharibu Dini na ni kutunga Shari´ah [mpya] ambako kunapingana na Shari´ah ya Allaah. Kunaharibu zaidi kuliko watu wa maasi, wafanyaji dhuluma na wauaji. Watu hawa hawasemi kuwa haya tuyafanyayo ni Dini ya Allaah. Lau wangelisema hivo watu wangeliwakadhibisha. Lakini watu hawa wanawadanganya watu na wanasema haya tuyafanyayo ni Dini ya Allaah pasina kujali hata kama itakuwa ni Ilhaad, uzindiki, kufuru na upotevu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/nani-mwenye-haki-ya-kuwaua-khawaarij/

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/149-150)
  • Imechapishwa: 26/08/2020