Swali: Je, inafaa kutaka msaada kutoka kwa jini muislamu juu ya kumtoa nje shaytwaan kutoka kwenye kiwiliwili cha mgonjwa muislamu?

Jibu: Haifai kwake kufanya hivo. Majini hatujui hali zao. Haitakikani kwenda mbali zaidi. Wanaweza kumvuta katika mambo ambayo mwisho wake si wenye kusifika. Anaweza kufikiria kuwa ni muislamu ilihali sio muislamu. Anaweza kuwa mnafiki. Ni kama watu ambapo miongoni mwao wako ambao ni Raafidhwah na wazushi. Allaah amesema kuhusu majini:

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا

”Na kwamba wako katika sisi wema na wako katika sisi kinyume na hivo; tumekuwa makundi ya njia mbalimbali.”[1]

Miongoni mwao wako ambao ni makafiri, waislamu, wanafiki, Raafidhwah, wazushi na Sunniyyuun. Sisi hatujui hali zao. Haitakikani kwa wasomaji kujiingiza katika jambo hilo.

[1] 72:11

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 04/10/2020